Ni bure, inakua haraka, na inafeed kubadilisha 20-30% ya chakula cha kawaida. Watu wengi Bahati/Nakuru wameianza juu ya bei ya feeds.
*1. Azolla ni nini?*
Ni mmea mdogo unaelea juu ya maji. Ina protein 25-30%, amino acids, minerals. Kuku, bata, ng'ombe, nguruwe, na samaki wanapenda.
Faida kubwa: Inafix nitrogen kutoka hewa, so haitaji fertilizer mingi.
*2. Jinsi ya kuanzisha Azolla pond:*
1. *Eneo*: Shadow 50%. Chini ya net ama chini ya miti. Jua kali = inakufa. 2m x 3m inatosha kuanzia.
2. *Pond*: Tengeneza bed na plastic dam liner. Weka matope 5cm + maji 10cm. Depth yote = 15cm tu.
3. *Soil + Mbolea*: Changanya mbolea ya ng'ombe iliyooza + DAP kidogo. pH iwe 5.5 - 7.0
4. *Seed*: Nunua Azolla "starter" 2kg. Tafuta kwa KEPHIS, KALRO, ama shamba la mtu aliyenalo. Tupa juu ya maji.
5. *Muda*: Wiki 2 imejaa pond yako. Kuanzia wiki 3 unavuna daily.
*3. Matunzo:*
1. *Maji*: Ongeza maji kila wiki 3-4. Usiachie ikauke.
2. *Vuna*: Kila siku toa 30% na wacha 70%. Ikiwa mingi sana inakufa chini. Tumia wavu.
3. *Mbolea*: Weka mbolea ya ng'ombe 1kg + DAP vijiko 2 kila wiki 2.
4. *Wadudu*: Slugs na snails wanakula Azolla. Weka majivu around pond.
*4. Jinsi ya kutoa kwa mifugo:*
1. *Kuku*: Changanya Azolla safi 20% + feeds 80%. Mayai yanaongezeka na yolk inakuwa yellow. Usipitishe 30% ama mayai yatakuwa na harufu.
2. *Ng'ombe*: Weka 1-2kg per cow daily ikichanganywa na dairy meal. Maziwa yanaongezeka 1-2L.
3. *Samaki*: Wala direct. Ni chakula number 1 kwa tilapia na catfish.
4. *Osha kwanza*: Osha Azolla ili uondoe mbolea iliyobaki.
*5. Gharama vs Faida:*
**Kitu** **Gharama**
**Pond ya 2x3m** 3k-5k liner + mbao
**Azolla seed 2kg** 1k-1.5k one time
**Vuna per day** 1-2kg fresh
**Akiba ya feed** 30% = ukiwa na kuku 500 unasave 8k/month
Inaanza kutoa faida after mwezi 1 tu.
*Makosa 2 ya kuepuka:*
1. *Jua kali direct* = Azolla inageuka brown na kufa
2. *Maji machafu* = inakaa na harufu na kuku wanakataa